102. Kazi Yangu Ikiisha (When my life work is ended)
102. Kazi Yangu Ikiisha (When my life work is ended)
1.
Kazi yangu ikiisha, nami
nikiokoka;
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi
nifikapo ng’amboni;
Atakuwa wa kwanza
kunilaki.
Nitamjua, nitamjua,
nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua,
kwa alama za misumari.
2.
Furaha nitapata nikiona
makao
Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu mwokozi kwa
rehema na pendo
Vilivyonipa pahali
Mbinguni.
3.
Nao waliokufa katika
Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake
huko Mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi
kwanza.
4.
Milangoni mwa mji Bwana
atanipisha,
Pasipo machozi wala
huzuni.
Nitauimba wimbo wa
milele; lakini
Nataka kumwona Mwokozi
kwanza.
Comments
Post a Comment