103. Kaa Nami (Abide with me)
103. Kaa Nami (Abide
with me)
1.
Kaa nami, ni usiku tena;
Usiniache gizani, Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu, kaa
nami.
2.
Siku zetu hazikawi
kwisha,
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi,
Usiye na mwisho kaa
nami.
3.
Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa
kunifaa;
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe Bwana, kaa
nami.
4.
Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote, si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako, kaa
nami.
5.
Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikie;
Nuru za mbinguni
hazikomi,
Siku zangu zote kaa
nami.
Comments
Post a Comment