105. Kuwatafuta (Seeking the lost)
105. Kuwatafuta (Seeking the lost)
1.
Kuwatafuta wasioweza,
Kuomba wamrejee Yesu,
Kuwaambia maneno yake,
“Njooni kwangu,
nawapenda”.
Nitakwenda, (kwenda),
niwatafute
Waongofu (wa Bwana)
wageuke,
Waingie (wote) katika
zizi
La Mkombozi (wetu)
Yesu kristo.
2.
Kuwatafuta wasioweza,
Waonyeshwe Mwokozi wetu,
Kuwaongoza, wapate wote
Uzima wa milele.
3.
Kazi hiyo nataka
kufanya,
Leo nimesikia mwito
Kuwainua waangukao,
Waletwe kwake Yesu njia.
Comments
Post a Comment