106. Mungu Awe Nanyi Daima (God be with you till we meet again)
106. Mungu Awe Nanyi
Daima (God be with you till we meet again)
1.
Mungu awe nanyi daima,
Hata twonane ya pili,
Awachunge kwa fadhili,
Mungu awe nanyi daima.
Hata twonane huko juu,
Hata twonane kwake
kwema;
Hata twonane huko juu,
Mungu awe nanyi daima.
2.
Mungu awe nanyi daima;
Ziwafunike mbawaze,
Awalishe, awakuze;
Mungu awe nanyi daima.
3.
Mungu awe nanyi daima;
Kila wakati wa shani
Awalinde hifadhini;
Mungu awe nanyi daima.
4.
Mungu awe nanyi daima;
Awabarikie sana,
Awapasulie kina;
Mungu awe nanyi daima.
Comments
Post a Comment