107. Ewe, Baba Wa Mbinguni (Heavenly Father, hear our prayer)
107. Ewe, Baba Wa
Mbinguni (Heavenly Father, hear our prayer)
1.
Ewe, Baba wa Mbinguni,
Usikie twombalo
Hapa chini duniani,
Na uwe radhi nalo
Ee Mungu, bariki
Ndugu hawa wawili!
Ee Mungu, bariki
Ndugu hawa wawili!
2.
Watu hawa mbele zako,
Na mbele ya kanisa;
Watimize Neno lako
Wanakutana sasa.
3.
Kama Yesu na Kanisa,
Ni mmoja, na hivyo,
Watu hawa wape sasa
Wawe mmoja vivyo
4.
Walinde, Bwana, daima,
Wabariki nyumbani
Uwape nyingi salama
Humu ulimwenguni.
5.
Wabariki, ewe Bwana,
Watu hawa wawili,
Wape upaji wa wana,
Wafurahishwe kweli.
6.
Siku zao duniani
Zitakapopungua,
Wape kurithi Mbinguni
Mema ya kwendelea.
Comments
Post a Comment