108. Twenende Sayuni (We're marching to Zion)
108. Twenende Sayuni (We're marching to Zion)
1.
Mpendao Bwana
Ije raha yenu!
Imbeni nyimbo za raha
Wa ibada yenu.
Twenende Sayuni,
Mji mzuri Sayuni;
Twenende juu Sayuni
Ni maskani ya Mungu.
2.
Wasiimbe wao
Wasioamini,
Watoto wa Mungu ndio
Waimbao chini.
3.
Twaona rohoni
Baraka za Mungu,
Tusijafika Mbinguni
Kwenye utukufu.
4.
Tutakapo mwona
Masumbuko basi,
Huwa maji ya uzima,
Anasa halisi.
5.
Tupaaze sauti,
Na fute machozi,
Twenenda kwa Imanweli
Naye ni Mwokozi.
Comments
Post a Comment