110. Mapya ni Mapenzi Hayo (New every morning is the love)
110. Mapya ni Mapenzi
Hayo (New every morning is the love)
1.
Mapya ni mapenzi hayo,
Asubuhi tuonayo,
Saa za giza hulindwa
Kwa uzima kuamshwa.
2.
Kila siku, mapya pia
Rehema, wema, na afya,
Wokovu, na msamaha,
Mawazo mema, furaha.
3.
Tukijitahidi leo
Na mwendo utupasao,
Mungu atatueleza
Yatakayompendeza.
4.
Mambo yetu ya dunia
Mungu atayang’aria,
Matata atageuza
Yawe kwetu ya baraka.
5.
Yaliyo madogo, haya
Mungu tukimfanyia,
Yatosha: tutafaidi
Huvuta kwake zaidi.
6.
Ewe Bwana, siku zote,
Tusaidie kwa yote:
Mwendo wetu wote vivyo,
Uwe kama tuombavyo.
Comments
Post a Comment