112. Nilikupa Wewe Maisha Yangu (I gave my life for Thee)
112. Nilikupa Wewe
Maisha Yangu (I gave my life for Thee)
1.
Nilikupa wewe
Damu ya moyoni,
Ili wokolewe,
Winuke ufuni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?
2.
Nilikupa miaka
Yangu duniani
Upate inuka,
Kuishi Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini:
3.
Niliacha nuru
Za Baba, Mbinguni,
Kwingia taabu
Za ulimwenguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?
4.
Niliteswa sana,
Mateso kifoni,
Usije yaona
Hayo ya motoni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?
5.
Nimekuletea
Huku duniani
Upendo na afya
Zatoka Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?
6.
Nipe siku zako,
Udumu mwangani;
Na taabu yako,
Wingie rahani
Nafsi, pendo, mali,
Twae Imanweli.
Comments
Post a Comment