113. Ni Mfalme wa Mapenzi (The King of love my Shepherd is)
113. Ni Mfalme wa
Mapenzi (The King of love my Shepherd is)
1.
Ni Mfalme wa mapenzi
Ndiye anichungaye,
Sipungukiwi, hawezi.
Kunipoteza yeye.
2.
Kando ya maji mazima
Yeye huniongoza
Katika malisho mema
Daima hunilaza.
3.
Mara nyingi hupotea
Kwa ukaidi wangu,
Naye huniandamia,
Hunirudisha kwangu.
4.
Uvulini mwa mauti,
Sichi hatari kamwe,
Wewe Bwana huniachi,
Mwokozi wangu Wewe.
5.
Waniandikia meza
Neema kwako tele.
Kwa Wewe, yote naweza.
Na msalaba mbele.
6.
Kamwe hautapungua
Uule wema wako;
Mwisho, atanichukua,
Juu, niimbe kwako.
Comments
Post a Comment