114. Bwana Mungu, Nashangaa Kabisa (How great thou art)
114. Bwana Mungu,
Nashangaa Kabisa (How great thou art)
1.
Bwana Mungu, nashangaa
kabisa
Nikitazama kama vilivyo
Nyota, ngurumo, vitu
vingi vyote
Viumbwavyo kwa uwezo
wako.
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi Wewe ulivyo
Mkuu,
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi Wewe ulivyo
Mkuu.
2.
Nikitembea pote duniani,
Ndege huimba, nawasikia,
Milima hupendeza macho
sana,
Upepo nao nafurahia.
3.
Nikikumbuka kama Wewe
Mungu
Ulivyompeleka Mwanao,
Afe azichukue dhambi
zetu,
Kuyatambua ni vigumu
mno.
4.
Yesu Mwokozi utakaporudi
Kunichukua kwenda
Mbinguni,
Nitashukuru na kwimba
milele,
Wote wajue jinsi ulivyo.
Comments
Post a Comment