121. Liko Lango Moja Wazi (The gate ajar for me)

121. Liko Lango Moja Wazi (The gate ajar for me)

 

1.   

Liko lango moja wazi,

Ni lango la mbinguni;

Na wote waingiao

Watapata nafasi.

 

Lango ndiye Yesu Bwana

Wote waingie kwake,

Lango! Lango

La Mbinguni ni wazi.

 

2.   

Yesu ndiye lango hili,

Hata sasa ni wazi,

Kwa wakubwa na wadogo,

Tajiri na maskini.

 

3.   

Hili ni lango la raha,

Ni lango la rehema;

Kila mtu apitaye

Hana majonzi tena.

 

4.   

Tukipita lango hili

Tutatua mizigo,

Tuliochukua kwanza,

Tutavikwa uzima.

 

5.   

Hima ndugu tuingie

Lango halijafungwa,

Likifungwa mara moja

Halitafunguliwa

Comments

Popular posts from this blog

101. Twonane Milele (In the sweet by-and-by)

102. Kazi Yangu Ikiisha (When my life work is ended)

104. Twasoma ni Njema Sana (There is a better world they say)