122. Bwana Yesu
122. Bwana Yesu
1.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona unaumia? Unateseka
sana,
Kwa ajili ya kuomba,
Waomba na jasho jingi
likageuka damu.
Kumbe! Ni dhambi zangu
zinazokuumiza.
Bwana wangu, Mungu
wangu,
Mimi leo, naja kwako
Ili niziungame.
2.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona unaumia, na mizigo
mizito?
Umejitwalia wewe,
msalaba mabegani
Kwa ajili ya watu.
3.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona unatukanwa,
wawambwa kama mwizi,
Bila kosa ukalia, Baba
yangu, wasamehe,
Chukua roho yangu.
4.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Muda ulipofika, nchi
ikawa giza,
Mbinguni pakatulia,
Angani pakawa kimya,
Watu wakaogopa.
5.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Jinsi ulivyoumwa,
ukamwomba Baba,
Leo umeshinda kifo, sasa
wapaa Mbinguni,
Naimba, Haleluya.
Comments
Post a Comment