Posts

101. Twonane Milele (In the sweet by-and-by)

101. Twonane Milele (In the sweet by-and-by)   1.     Nyimbo na tuziimbe tena Za alivyotupenda mbele; Kwa damu ya thamani sana! Mbinguni twonane milele.   Twonane milele, Twonane bandarini kule; Twonane milele, Twonane bandarini kule.   2.     Hupozwa kila aoshwaye, Kwa damu ya Kondoo yule; Ataishi afurahiye Vya Yesu mbinguni milele.   3.     Hata sasa hufurahia Tamu yake mapenzi yale, Je, kwake tukifikilia, Kutofarakana milele?   4.     Twende mbele kwa jina lake, Hata aje mwokozi yule, Atatukaribisha kwake, Tutawale naye milele.   5.     Sauti zetu tuinue Kumsifu Mwokozi yule, Ili watu wote wajue Wokovu u kwake milele.

102. Kazi Yangu Ikiisha (When my life work is ended)

  102. Kazi Yangu Ikiisha (When my life work is ended)   1.     Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka; Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni; Atakuwa wa kwanza kunilaki.   Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.   2.     Furaha nitapata nikiona makao Bwana aliyotuandalia; Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo Vilivyonipa pahali Mbinguni.   3.     Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu; Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza.   4.     Milangoni mwa mji Bwana atanipisha, Pasipo machozi wala huzuni. Nitauimba wimbo wa milele; lakini Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

103. Kaa Nami (Abide with me)

103. Kaa Nami (Abide with me)   1.     Kaa nami, ni usiku tena; Usiniache gizani, Bwana; Msaada wako haukomi; Nili peke yangu, kaa nami.   2.     Siku zetu hazikawi kwisha, Sioni la kunifurahisha; Hakuna ambacho hakikomi, Usiye na mwisho kaa nami.   3.     Nina haja nawe kila saa; Sina mwingine wa kunifaa; Mimi nitaongozwa na nani Ila wewe Bwana, kaa nami.   4.     Sichi neno uwapo karibu; Nipatalo lote, si taabu; Kifo na kaburi haviumi; Nitashinda kwako, kaa nami.   5.     Nilalapo nikuone wewe, Gizani mote nimulikie; Nuru za mbinguni hazikomi, Siku zangu zote kaa nami.

104. Twasoma ni Njema Sana (There is a better world they say)

104. Twasoma ni Njema Sana (There is a better world they say)    1.     Twasoma, ni njema sana Mbinguni, kwa Bwana; Twasoma, dhambi hapana, Mbinguni kwa Bwana; Malaika wema wako, Vinanda vizuri viko, Na majumba tele yako, Mbinguni kwa Bwana.   2.     Siku zote ni mchana, Ni nchi ya raha; Wala machozi hapana, Ni nchi ya raha; Walioko wauona Uso wa Mwokozi, tena Jua jingine hapana, Ni nchi ya raha.   3.     Nyama na vitu viovu Havimo kabisa; Kifo nacho, na ubovu, Havimo kabisa. Ni watakatifu wote, Wameoshwa dhambi zote; Wasiosafiwa wote Hawamo kabisa.   4.     Tuna dhambi, pia sote, Mwokozi akafa; Kwake tutaoshwa zote, Mwokozi akafa; Kwake twapata wokovu, Tutawona utukufu; Mbinguni tutamsifu; Mwokozi akafa.   5.     Baba, mama, ndugu zetu, Twendeni kwa Bwana; Huku chini sio kwetu, Twendeni kwa Bwana; Tusishikwe na dunia, Na dhambi kutulemea; Tutupe vya chini pia, ...

105. Kuwatafuta (Seeking the lost)

  105. Kuwatafuta (Seeking the lost)   1.     Kuwatafuta wasioweza, Kuomba wamrejee Yesu, Kuwaambia maneno yake, “Njooni kwangu, nawapenda”.   Nitakwenda, (kwenda), niwatafute Waongofu (wa Bwana) wageuke, Waingie (wote) katika zizi La Mkombozi (wetu) Yesu kristo.   2.     Kuwatafuta wasioweza, Waonyeshwe Mwokozi wetu, Kuwaongoza, wapate wote Uzima wa milele.   3.     Kazi hiyo nataka kufanya, Leo nimesikia mwito Kuwainua waangukao, Waletwe kwake Yesu njia.

106. Mungu Awe Nanyi Daima (God be with you till we meet again)

106. Mungu Awe Nanyi Daima (God be with you till we meet again)   1.     Mungu awe nanyi daima, Hata twonane ya pili, Awachunge kwa fadhili, Mungu awe nanyi daima.   Hata twonane huko juu, Hata twonane kwake kwema; Hata twonane huko juu, Mungu awe nanyi daima.   2.     Mungu awe nanyi daima; Ziwafunike mbawaze, Awalishe, awakuze; Mungu awe nanyi daima.   3.     Mungu awe nanyi daima; Kila wakati wa shani Awalinde hifadhini; Mungu awe nanyi daima.   4.     Mungu awe nanyi daima; Awabarikie sana, Awapasulie kina; Mungu awe nanyi daima.

107. Ewe, Baba Wa Mbinguni (Heavenly Father, hear our prayer)

107. Ewe, Baba Wa Mbinguni (Heavenly Father, hear our prayer)   1.     Ewe, Baba wa Mbinguni, Usikie twombalo Hapa chini duniani, Na uwe radhi nalo   Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili!   2.     Watu hawa mbele zako, Na mbele ya kanisa; Watimize Neno lako Wanakutana sasa.   3.     Kama Yesu na Kanisa, Ni mmoja, na hivyo, Watu hawa wape sasa Wawe mmoja vivyo   4.     Walinde, Bwana, daima, Wabariki nyumbani Uwape nyingi salama Humu ulimwenguni.   5.     Wabariki, ewe Bwana, Watu hawa wawili, Wape upaji wa wana, Wafurahishwe kweli.   6.     Siku zao duniani Zitakapopungua, Wape kurithi Mbinguni Mema ya kwendelea.